61
subscribers
Can't Join? t.me/netprofitfx
61
subscribers
Updated: Nov 17, 2025
BACKUP CHANNEL đ„·đœ
OFFICIAL CHANNEL : @NPFXSIGNALS
WEBSITE : NETPROFITFX.COM
netprofitfx
May 14, 2025, 6:25
TAARIFA MUHIMU KUHUSU ANAYEDAIWA KUWA MTOTO WA MCHUNGAJI .
Nianze kwa kusema mada ya huyu imekuwa kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii lakini watu wengi hawajui usahihi wa habari hiyo , hapa nimeona niandike kidogo taarifa sahihi kuhusu huyo anayedaiwa kuwa ni mtoto wa mchungaji .
Jina la binti ni Roselande Bélony?
Roselande Bélony ni mtangazaji wa redio na televisheni kutoka Haiti, aliyefanya kazi na Radio Télé Pacific, mojawapo ya vituo maarufu vya habari nchini humo. Alikuwa sehemu ya kipindi maarufu kiitwacho "Viv Ayiti", ambacho huzungumzia masuala ya kijamii, maendeleo na maisha ya kila siku nchini Haiti.
Kuhusu tukio linalosambaa sasa :
Mwishoni mwa mwaka 2023 (takribani mwezi Desemba), Roselande alijikuta kwenye kashfa ya mitandaoni baada ya video ya faragha inayodaiwa kumhusisha kusambazwa mtandaoni. Video hiyo ilienea kwa kasi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, na kusababisha maumivu makubwa ya kisaikolojia na kijamii kwake.
Athari Zilizojitokeza:
1. Kujiuzulu kutoka kazi yake: Roselande alilazimika kuacha kazi Radio Télé Pacific kutokana na presha na aibu kubwa iliyotokana na video hiyo.
2. Madhara ya kisaikolojia: Aliathirika kwa kiasi kikubwa kisaikolojia kutokana na matusi, kejeli, na unyanyasaji wa mitandaoni alioupata kutoka kwa jamii.
3. Kuibuka kwa mjadala wa kitaifa kuhusu "cyberviolence" (unyanyasaji wa kidijitali): Tukio lake lilizua mjadala mkubwa Haiti kuhusu usalama wa wanawake mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia kupitia mitandao, na haki ya faragha.
JE YEYE NI MTOTO WA MCHUNGAJI ??
Hapana, hakuna ushahidi wowote wa kuaminika unaothibitisha kwamba Roselande Bélony ni mtoto wa mchungaji.
Ukweli kuhusu hilo:
Taarifa rasmi kutoka vyombo vya habari vya Haiti (kama Le National na Radio Mélodie Inter) hazimtambui kama mtoto wa mchungaji.
Madai ya âmtoto wa mchungajiâ yameibuka baada ya video kuanza kusambazwa katika nchi nyingine, hasa Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, n.k.), ambapo watu hawamfahamu kiundani.
Inawezekana jina au taswira yake limehusishwa kimakosa na mtu mwingine, au baadhi ya watu wameongeza hadithi ya âmtoto wa mchungajiâ ili kuchochea hisia za kidini na maadili.
Sababu za kuchanganyikiwa:
1. Tafsiri isiyo sahihi ya tukio la Haiti kutoka lugha ya Kifaransa/Kikreyol kwenda Kiswahili.
2. Kutokuwepo kwa uthibitisho rasmi kwenye video yenyewe.
3. Tabia ya mitandao kuunganisha âskendoâ na taswira za kidini ili kuvutia watazamaji zaidi.
Kwa hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Roselande Bélony si mtoto wa mchungaji, bali ni mwanahabari wa Haiti aliyekuwa akifanya kazi Radio Télé Pacific.
KWANINI TUKIO HILI LIVUME UPYA WAKATI HUU ??
1. Mitandao ya kijamii âhufufuaâ matukio
Mara nyingi, video au habari za zamani huchukuliwa tena na kusambazwa na watumiaji wapya wa mitandao (TikTok, Facebook, WhatsApp, Telegram n.k.). Baadhi ya sababu ni:
Watu wapya wanaiona kwa mara ya kwanza
Kuna kurasa au akaunti zinazochimba "skendo za zamani"
Mitandao huchochea maudhui yenye hisia kali (aibu, hasira, udadisi)
2. Watu wengine maarufu wanaweza kuhusishwa kimakosa
Mara nyingine, watu huanza kufikiri kwamba tukio hilo linahusiana na mtu wanayemjua kwa sasa (kwa mfano, binti wa mchungaji fulani), hata kama si kweli. Hii huchochea utafutaji na mijadala mpya.
3. Lugha tofauti na mazingira mapya
Roselande ni kutoka Haiti, anazungumza Kifaransa/Kikreyol. Lakini sasa video hiyo imeingia katika muktadha wa Kiswahili, ikizua mjadala mpya kwenye nchi kama Tanzania au Kenya. Hii hufanya ionekane kama tukio jipya.
4. Uvumi na muktadha wa udini/maadili
Maneno kama âmtoto wa mchungajiâ yameambatanishwa na tukio hili, hata kama hayana ushahidi. Hili linafanya watu kuwa na hamu ya kujua na kusambaza zaidi â kwa sababu linaingiliana na maadili na dini.
Maoni yangu binafsi
Huu hapa ni ujumbe wa mfano wa kiroho na kimaadili unaoweza kutumia ili kuwaonesha watu jinsi shetani hutumia udanganyifu kuchafua kanisa, akiwasingizia hata watu wasiohusika:
netprofitfx
May 14, 2025, 6:23
netprofitfx
May 14, 2025, 5:03
Wadau wagumu sana, kabisa mmegoma kussuport hata vocha tuu duhđ§đ§đ§
netprofitfx
May 9, 2025, 8:20
Rais Thomas Sankara alipata kuwa mwanamapinduzi msema ukweli hata katika mikutano ya Umoja wa Afrika OAU Ambapo alikuwa akiwashauri viongozi wenzake wa Afrika katika umoja huo kukataa kulipa mikopo mikubwa ya IMF na world bank na hii ni kutokana na ongezeko kubwa la riba katika mikopo hiyo na badala yake aliwashauri viongozi hao kuanza kuanzisha viwanda vya kutosha na kuchukua wataalam wetu wakasome ulaya na kisha kurudisha nyumbani utaalam wao.Thomas sankara anakumbukwa kwa maneno yake mazito na kauli mbiu yake ya â To our homeland or death we shall winâ yaani kwa ajili ya taifa letu tupo tayar kufa ili tushinde.Thomas sankara aliamini kuwa Afrika Ina masoko ya kutosha ya kuuza bidhaa zake na kama nchi hizi zitaungana basi umasikini utaisha Afrika.
Thomas Sankara ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake alianzisha viwanda vya nguo na alisisitiza sana wananchi wa Burkinafaso kufanya kazi kwa bidii ili kuikomboa nchi hiyo katika umasikini.
Misukosuko katika uongozi wa Rais Thomas Sankara ilianza kipindi Cha mwaka 1986 ambapo kulitokea mgomo mkubwa wa walimu na hivyo Rais Thomas Sankara aliwafukuza kazi zaidi ya walimu 1200 na kisha kuwapatia mafunzo vijana waliomaliza elimu ya juu ili wakawafundishe wanafunzi katika kipindi hiko cha mpito na hapo ndipo migogoro ilipoanza katika nchi ya Burkinafaso na wasomi wengi wakiupinga uamuzi wake huo.
KUPINDULIWA NA KUUWAWA KWA RAIS THOMAS SANKARA
Wataalam wa siasa wanasema Rais Thomas Sankara alikiona kifo chake na alikisubiri kwa sababu kipindi chote cha kutokueleweka kwake na nchi ya Ufaransa kwasababu Rais Thomas Sankara alipenda kushirikiana na mataifa mbalimbali bila kufungamana na upande wowote.Hali iliyopelekea watawala kutoka Ufaransa kukasirika kwani walitaka waendelee kulitawala taifa hilo katika ukoloni mambo Leo kwa kuhakikisha nchi ya Burkinafaso inaendelea kuwa ni soko la bidhaa kutoka Ufaransa na pia bajeti ya matumizi ya Nchi hiyo ikainufaishe nchi ya Ufaransa.Hivyo basi walimtumia rafiki wa Rais Thomas Sankara Bwana Braise Compare kuandaa mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara na hapo ndipo ikawa mwisho wa Rais Thomas Sankara. Tetesi za mauaji dhidi yake Rais Thomas Sankara alizipata, lakini hakuchukua hatua zozote kwani aliamini ubaya usitokee kwake bali utokee kwa wanaompinga.
Tarehe 15/10/1987 Rais Thomas Sankara aliuawa kikatili na kuzikwa usiku huo huo.Na kisha asubuhi yake Bwana Braise Compare rafiki wa karibu wa Rais Thomas Sankara alijitangaza kuwa Rais wa Nchi ya Burkinafaso.Rais Compare alitawala nchi ya Burkinafaso kwa miaka 27 hadi mwaka 2014.
Familia ya Rais Thomas Sankara ilifungua kesi ya mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara ambapo ilipofika mwaka 2022 ilithibitika katika mahakama ya Burkinafaso kuwa Rais Compare na wenzake 14 warishiriki katika mauaji ya Rais Thomas Sankara na Rais Compare alihukumiwa kifungo cha maisha jela.
netprofitfx
May 9, 2025, 5:11
#CHAKUSHANGAZA
Cleopa David Msuya alizaliwa tarehe 4 Januari 1931 katika kijiji cha Chomvu, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Makerere kuanzia mwaka 1952 hadi 1955. Baada ya hapo, alijihusisha na kazi za maendeleo ya jamii na huduma kwa wananchi vijijini kuanzia mwaka 1956 hadi 1964.
Kuanzia mwaka 1964, Msuya alihudumu kama Katibu Mkuu katika wizara mbalimbali: Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Utamaduni (1964â1965), Wizara ya Ardhi, Makazi na Maendeleo ya Maji (1965â1967), Wizara ya Mambo ya Uchumi na Mipango (1967â1970), na Wizara ya Fedha (1970â1972).
Mnamo tarehe 18 Februari 1972, aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na alihudumu hadi alipohamishiwa kuwa Waziri wa Viwanda mnamo tarehe 3 Novemba 1975. Baada ya kuhudumu kwa miaka mitano kama Waziri wa Viwanda, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mnamo Novemba 1980, nafasi aliyoshikilia hadi Februari 1983. Baadaye alirudi tena kuwa Waziri wa Fedha kutoka Februari 1983 hadi Novemba 1985.
Mnamo tarehe 6 Novemba 1985, alipewa jukumu jipya akiwa Waziri wa Fedha, Mambo ya Uchumi na Mipango hadi Machi 1989. Kisha alirudi kuwa Waziri wa Fedha tena kuanzia Machi 1989 hadi Desemba 1990, na baadaye kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Machi 1990 hadi Desemba 1994.
Mwaka 1994, aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili, na pia kuhudumu kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi Novemba 1995. Katika uchaguzi wa Bunge wa mwaka 1995, alichaguliwa tena kuwa Mbunge na alihudumu hadi alipojitokeza kustaafu rasmi tarehe 29 Oktoba 2000.
Baada ya kustaafu, Msuya aliendelea kuwa mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kufikia mwaka 2006 alikuwa bado ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Pia alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo la Kilimanjaro.
Mnamo Oktoba 23, 2019, akiwa na umri wa miaka 88, Cleopa Msuya aliteuliwa na Rais Hayati John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi (Chancellor wa Ardhi Institute).
Mzee Msuya amefariki Jana tarehe 07/05/2025 katika hospitali ya NZENA alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo ,alikuwa akiugua mda mrefu amepita JKCI na London Uingereza, Bwana Ametoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe ,wa ina lillah raajun
netprofitfx
May 9, 2025, 5:11
netprofitfx
September 30, 2024, 14:59
3.5mm With Mic Super Bass Music In Ear Stereo Earphone Earbuds 1.2m Black Earphone For Samsung more...
Sale Price đ 2.36$ 3.47$
Rating: âââââ
netprofitfx
May 3, 2025, 16:08
netprofitfx
May 3, 2025, 13:30
netprofitfx
May 1, 2025, 10:31
Afu leo mnitumie basi vocha ili nimalizie hii story.... hamuoni hata huruma nimeandika gazeti lote hilo...0627408679
Tumeni laki laki hizo