off img

Can't Join? t.me/kapzkorner

subscribers number

1 153

subscribers

Kapz Korner

Updated: Nov 7, 2025


My Original Apu Art

Country Rank 8415 ↓17
Country United States
Language English

Latest Posts

kapzkorner

May 9, 2025, 5:11

#CHAKUSHANGAZA
Cleopa David Msuya alizaliwa tarehe 4 Januari 1931 katika kijiji cha Chomvu, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Makerere kuanzia mwaka 1952 hadi 1955. Baada ya hapo, alijihusisha na kazi za maendeleo ya jamii na huduma kwa wananchi vijijini kuanzia mwaka 1956 hadi 1964.

Kuanzia mwaka 1964, Msuya alihudumu kama Katibu Mkuu katika wizara mbalimbali: Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Utamaduni (1964–1965), Wizara ya Ardhi, Makazi na Maendeleo ya Maji (1965–1967), Wizara ya Mambo ya Uchumi na Mipango (1967–1970), na Wizara ya Fedha (1970–1972).

Mnamo tarehe 18 Februari 1972, aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na alihudumu hadi alipohamishiwa kuwa Waziri wa Viwanda mnamo tarehe 3 Novemba 1975. Baada ya kuhudumu kwa miaka mitano kama Waziri wa Viwanda, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mnamo Novemba 1980, nafasi aliyoshikilia hadi Februari 1983. Baadaye alirudi tena kuwa Waziri wa Fedha kutoka Februari 1983 hadi Novemba 1985.

Mnamo tarehe 6 Novemba 1985, alipewa jukumu jipya akiwa Waziri wa Fedha, Mambo ya Uchumi na Mipango hadi Machi 1989. Kisha alirudi kuwa Waziri wa Fedha tena kuanzia Machi 1989 hadi Desemba 1990, na baadaye kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Machi 1990 hadi Desemba 1994.

Mwaka 1994, aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili, na pia kuhudumu kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi Novemba 1995. Katika uchaguzi wa Bunge wa mwaka 1995, alichaguliwa tena kuwa Mbunge na alihudumu hadi alipojitokeza kustaafu rasmi tarehe 29 Oktoba 2000.

Baada ya kustaafu, Msuya aliendelea kuwa mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kufikia mwaka 2006 alikuwa bado ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Pia alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo la Kilimanjaro.

Mnamo Oktoba 23, 2019, akiwa na umri wa miaka 88, Cleopa Msuya aliteuliwa na Rais Hayati John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi (Chancellor wa Ardhi Institute).

Mzee Msuya amefariki Jana tarehe 07/05/2025 katika hospitali ya NZENA alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo ,alikuwa akiugua mda mrefu amepita JKCI na London Uingereza, Bwana Ametoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe ,wa ina lillah raajun

kapzkorner

September 30, 2024, 14:59

3.5mm With Mic Super Bass Music In Ear Stereo Earphone Earbuds 1.2m Black Earphone For Samsung more...

Sale Price 👉 2.36$ 3.47$

Rating: ⭐⭐⭐⭐⭐

kapzkorner

September 30, 2024, 14:58

DIY Wooden Book Nook Shelf Insert Kit Miniature Building Kits Bookshelf Magic Series Bookends Adult Birthday Gifts more...

Sale Price 👉 33.28$ 114.76$
📢📢📢 PRICE ALERT 📢📢📢

Rating: ⭐⭐⭐⭐⭐

kapzkorner

May 3, 2025, 16:08

#CHAKUSHANGAZA

Usaliti wa Rafiki: Kifo cha Thomas Sankara

Muuaji wa Rais wa zamani wa Burkina Faso, Thomas Sankara, hakuwa mtu wa mbali. Alikuwa rafiki yake wa utotoni, Blaise Compaoré. Wawili hawa walikua pamoja tangu wakiwa watoto, waliishi pamoja na hata kulelewa pamoja na baba yake Sankara. Urafiki wao ulikuwa wa karibu kiasi kwamba waliishi kama ndugu wa damu.

Baadaye, walijiunga pamoja na jeshi la Burkina Faso na kuendeleza ukaribu wao. Thomas Sankara alipofanikiwa kuwa Rais wa nchi hiyo, alimchagua rafiki yake huyo mkubwa, Blaise Compaoré, kuwa Makamu wa Rais wake. Uaminifu na upendo wa kindugu ulitawala kati yao—angalau ndivyo Sankara alivyodhani.

Siku tano kabla ya mauaji ya Sankara, walifanya sherehe pamoja; walikunywa na kucheza wakisherehekea tukio fulani muhimu. Lakini katika usiku huo wa furaha, Sankara alipokea taarifa ya siri kutoka kwa maafisa wa usalama wake kwamba Blaise Compaoré alikuwa ameandaa mpango wa kumuua.

Thomas Sankara aliisikia taarifa hiyo lakini hakuweza kuiamini. Vipi rafiki yake mkubwa? Mtu waliyeshirikiana maisha tangu utotoni? Mtu aliyemwamini sana kiasi cha kumfanya Makamu wake? Aliamini kuwa haiwezekani mtu wa karibu kiasi hicho awe na nia ya kumuua.

Lakini dunia hii imejaa usaliti. Hatimaye, tarehe 15 Oktoba 1987, Thomas Sankara aliuawa katika mapinduzi yaliyoongozwa na mtu aliyempenda kama ndugu – Blaise Compaoré. Sankara alipigwa risasi 11 kifuani na 4 kichwani na vijana waliotumwa na Compaoré.

Baada ya kutekeleza usaliti huo, Blaise Compaoré alichukua uongozi wa Burkina Faso na kuwa Rais kwa miaka 27. Hadi leo, bado anaishi nchini Ivory Coast na hajawahi kulipa gharama ya usaliti wake.

Huu ndio ukweli mchungu wa dunia: mara nyingi, anayekuangamiza si adui wa mbali, bali rafiki wa karibu.

Pumzika kwa amani, Thomas Sankara.

kapzkorner

May 3, 2025, 13:30

#CHAKUSHANGAZA
Hili ni jino la aliyekuwa mpigania uhuru na waziri mkuu wa zamani nchini Congo. Hayati Patrice Lumumba aliyeuawa mwaka 1961 kwa kupigwa risasi, kuzikwa kisha mwili wake kufukuliwa tena muda mfupi baadae katika tukio ambalo liliratibiwa na Askari wa kikoloni wa Ubelgiji wakiongozwa na Bw. Gerard Soete ambaye miaka 40 baadae alikiri kwa kusema. "Nilimkata Lumumba vipande 34! Niliukata kata mwili wa Lumumba, sehemu ngumu ya mwili wake tulitumia msumeno! na kisha kuumwagia tindikali katikati ya usiku wa manane wa Afirka. Hakuna kilichobakia zaidi ya meno machache na harufu kali. Nilioga mara tatu na kila wakati nilijiona mchafu!" Alihitimisha hivyo mzungu huyo mwenye roho mbaya ambaye nae kwa sasa ni marehemu.... Rest in Peace Patrice Lumumba. Ulidhurumiwa uhai kikatili mno kwa ajili ya nchi yako na Afrika kwa ujumla. Jina lako bado linaishi kwenye mioyo yetu wapenda amani na wakarimu wa Afrika. Ndio maana mpaka leo kuna barabara zetu na mitaa inaliheshimisha jina lako. Kuna barabara inaitwa LUMUMBA hapa Dar es salaam. Ni kumbukumbu yako....Rest In Paradise ..PATRICE emery LUMUMBA😭😭

kapzkorner

May 1, 2025, 10:31

Afu leo mnitumie basi vocha ili nimalizie hii story.... hamuoni hata huruma nimeandika gazeti lote hilo...0627408679
Tumeni laki laki hizo