2 113
subscribers
Can't Join? t.me/airdropbulll
2 113
subscribers
Updated: Aug 14, 2024
🪂 The House Of Legitimate Airdrop Calls 🪂
Disscusion group👇🏽
https://t.me/airdropbulllChat
Support 🫡
@LatinOsDz
Patience and consistency pay off. Remember that. 🪂
airdropbulll
August 10, 2024, 11:59
Spike Marketplace - Your Trusted Marketplace!
Find quality items sold by trusted members.Reliable products offered by reputable sellers. Shop smart, shop secure.
Telegram Spike Marketplace
https://t.me/spikemp
Join Us and Start Earning Big!
airdropbulll
August 9, 2024, 12:37
Spike is the HQ marketplace,where you can find tons of quality things sold by known and trusted members
Spike Telegram Marketplace
https://t.me/+rNvszWFIUvZjYjJl
Lounge @spikelounge
Gateway @spikemp
Make sure to join us if you want to make good money
airdropbulll
August 9, 2024, 8:58
PayPal, XBOX, OnlyFans (with balance) and Ticketmaster with upcoming tickets restocked
More stock coming we are still on vacation so please be patient for restocks 🙏 love you all ❤️
Shop link: memeshop.cc
Channel: @memeshop
Live stock updates: @memestockupdates
Support: @memeplugsupport
airdropbulll
May 14, 2025, 6:25
UJUMBE: “Mipango ya Shetani ya Kuchafua Kanisa”
Katika siku hizi za mwisho, shetani ameongeza ujanja na hila zake ili kulichafulia jina kanisa la Kristo. Amekuwa akitumia teknolojia, mitandao ya kijamii, na lugha za uchochezi ili kueneza aibu, fitina, na uongo — kwa lengo la kudhoofisha imani ya watu na kuharibu heshima ya wokovu.
Mfano ni kusambazwa kwa skendo ya video chafu inayodaiwa kumhusisha “mtoto wa mchungaji”, jambo lililowashtua wengi na kuvuruga nafsi dhaifu. Lakini baada ya utafiti wa kina, imethibitika kuwa binti huyo si mtoto wa mchungaji bali ni mwanahabari kutoka Haiti aitwaye Roselande Bélony.
Huu ni ushahidi wa wazi wa hila za shetani — kutunga, kuchanganya watu, na kutumia jina la kanisa ili kueneza kejeli, aibu na chuki. Biblia inasema:
> “Shetani, adui yenu, huzunguka-zunguka kama simba angurumaye, akitafuta mtu wa kummeza.”
— 1 Petro 5:8
Ni wajibu wetu kama waamini:
Kuchunguza kila habari kwa hekima na kweli
Kuepuka kusambaza mambo yasiyojulikana chanzo chake
Kusimama upande wa haki na rehema badala ya hukumu za haraka
airdropbulll
May 14, 2025, 6:25
TAARIFA MUHIMU KUHUSU ANAYEDAIWA KUWA MTOTO WA MCHUNGAJI .
Nianze kwa kusema mada ya huyu imekuwa kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii lakini watu wengi hawajui usahihi wa habari hiyo , hapa nimeona niandike kidogo taarifa sahihi kuhusu huyo anayedaiwa kuwa ni mtoto wa mchungaji .
Jina la binti ni Roselande Bélony?
Roselande Bélony ni mtangazaji wa redio na televisheni kutoka Haiti, aliyefanya kazi na Radio Télé Pacific, mojawapo ya vituo maarufu vya habari nchini humo. Alikuwa sehemu ya kipindi maarufu kiitwacho "Viv Ayiti", ambacho huzungumzia masuala ya kijamii, maendeleo na maisha ya kila siku nchini Haiti.
Kuhusu tukio linalosambaa sasa :
Mwishoni mwa mwaka 2023 (takribani mwezi Desemba), Roselande alijikuta kwenye kashfa ya mitandaoni baada ya video ya faragha inayodaiwa kumhusisha kusambazwa mtandaoni. Video hiyo ilienea kwa kasi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, na kusababisha maumivu makubwa ya kisaikolojia na kijamii kwake.
Athari Zilizojitokeza:
1. Kujiuzulu kutoka kazi yake: Roselande alilazimika kuacha kazi Radio Télé Pacific kutokana na presha na aibu kubwa iliyotokana na video hiyo.
2. Madhara ya kisaikolojia: Aliathirika kwa kiasi kikubwa kisaikolojia kutokana na matusi, kejeli, na unyanyasaji wa mitandaoni alioupata kutoka kwa jamii.
3. Kuibuka kwa mjadala wa kitaifa kuhusu "cyberviolence" (unyanyasaji wa kidijitali): Tukio lake lilizua mjadala mkubwa Haiti kuhusu usalama wa wanawake mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia kupitia mitandao, na haki ya faragha.
JE YEYE NI MTOTO WA MCHUNGAJI ??
Hapana, hakuna ushahidi wowote wa kuaminika unaothibitisha kwamba Roselande Bélony ni mtoto wa mchungaji.
Ukweli kuhusu hilo:
Taarifa rasmi kutoka vyombo vya habari vya Haiti (kama Le National na Radio Mélodie Inter) hazimtambui kama mtoto wa mchungaji.
Madai ya “mtoto wa mchungaji” yameibuka baada ya video kuanza kusambazwa katika nchi nyingine, hasa Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, n.k.), ambapo watu hawamfahamu kiundani.
Inawezekana jina au taswira yake limehusishwa kimakosa na mtu mwingine, au baadhi ya watu wameongeza hadithi ya “mtoto wa mchungaji” ili kuchochea hisia za kidini na maadili.
Sababu za kuchanganyikiwa:
1. Tafsiri isiyo sahihi ya tukio la Haiti kutoka lugha ya Kifaransa/Kikreyol kwenda Kiswahili.
2. Kutokuwepo kwa uthibitisho rasmi kwenye video yenyewe.
3. Tabia ya mitandao kuunganisha “skendo” na taswira za kidini ili kuvutia watazamaji zaidi.
Kwa hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Roselande Bélony si mtoto wa mchungaji, bali ni mwanahabari wa Haiti aliyekuwa akifanya kazi Radio Télé Pacific.
KWANINI TUKIO HILI LIVUME UPYA WAKATI HUU ??
1. Mitandao ya kijamii “hufufua” matukio
Mara nyingi, video au habari za zamani huchukuliwa tena na kusambazwa na watumiaji wapya wa mitandao (TikTok, Facebook, WhatsApp, Telegram n.k.). Baadhi ya sababu ni:
Watu wapya wanaiona kwa mara ya kwanza
Kuna kurasa au akaunti zinazochimba "skendo za zamani"
Mitandao huchochea maudhui yenye hisia kali (aibu, hasira, udadisi)
2. Watu wengine maarufu wanaweza kuhusishwa kimakosa
Mara nyingine, watu huanza kufikiri kwamba tukio hilo linahusiana na mtu wanayemjua kwa sasa (kwa mfano, binti wa mchungaji fulani), hata kama si kweli. Hii huchochea utafutaji na mijadala mpya.
3. Lugha tofauti na mazingira mapya
Roselande ni kutoka Haiti, anazungumza Kifaransa/Kikreyol. Lakini sasa video hiyo imeingia katika muktadha wa Kiswahili, ikizua mjadala mpya kwenye nchi kama Tanzania au Kenya. Hii hufanya ionekane kama tukio jipya.
4. Uvumi na muktadha wa udini/maadili
Maneno kama “mtoto wa mchungaji” yameambatanishwa na tukio hili, hata kama hayana ushahidi. Hili linafanya watu kuwa na hamu ya kujua na kusambaza zaidi – kwa sababu linaingiliana na maadili na dini.
Maoni yangu binafsi
Huu hapa ni ujumbe wa mfano wa kiroho na kimaadili unaoweza kutumia ili kuwaonesha watu jinsi shetani hutumia udanganyifu kuchafua kanisa, akiwasingizia hata watu wasiohusika:
airdropbulll
May 14, 2025, 6:23
airdropbulll
May 14, 2025, 5:03
Wadau wagumu sana, kabisa mmegoma kussuport hata vocha tuu duh🧐🧐🧐
airdropbulll
May 13, 2025, 2:53
#CHAKUSHANGAZA
Charles Hilary (kushoto) na Julius Nyaisanga enzi za RTD miaka ya 1980.
Enzi hizo R.T.D charless Hilary akitangaza taalifa ya habar na Nyaisanga akitangaza kipindi Cha misakato na bima Yako dah wee acha tu mwenyezi mungu awapumzishe Kwa amani🙏
airdropbulll
May 9, 2025, 8:20
Rais Thomas Sankara alipata kuwa mwanamapinduzi msema ukweli hata katika mikutano ya Umoja wa Afrika OAU Ambapo alikuwa akiwashauri viongozi wenzake wa Afrika katika umoja huo kukataa kulipa mikopo mikubwa ya IMF na world bank na hii ni kutokana na ongezeko kubwa la riba katika mikopo hiyo na badala yake aliwashauri viongozi hao kuanza kuanzisha viwanda vya kutosha na kuchukua wataalam wetu wakasome ulaya na kisha kurudisha nyumbani utaalam wao.Thomas sankara anakumbukwa kwa maneno yake mazito na kauli mbiu yake ya “ To our homeland or death we shall win” yaani kwa ajili ya taifa letu tupo tayar kufa ili tushinde.Thomas sankara aliamini kuwa Afrika Ina masoko ya kutosha ya kuuza bidhaa zake na kama nchi hizi zitaungana basi umasikini utaisha Afrika.
Thomas Sankara ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake alianzisha viwanda vya nguo na alisisitiza sana wananchi wa Burkinafaso kufanya kazi kwa bidii ili kuikomboa nchi hiyo katika umasikini.
Misukosuko katika uongozi wa Rais Thomas Sankara ilianza kipindi Cha mwaka 1986 ambapo kulitokea mgomo mkubwa wa walimu na hivyo Rais Thomas Sankara aliwafukuza kazi zaidi ya walimu 1200 na kisha kuwapatia mafunzo vijana waliomaliza elimu ya juu ili wakawafundishe wanafunzi katika kipindi hiko cha mpito na hapo ndipo migogoro ilipoanza katika nchi ya Burkinafaso na wasomi wengi wakiupinga uamuzi wake huo.
KUPINDULIWA NA KUUWAWA KWA RAIS THOMAS SANKARA
Wataalam wa siasa wanasema Rais Thomas Sankara alikiona kifo chake na alikisubiri kwa sababu kipindi chote cha kutokueleweka kwake na nchi ya Ufaransa kwasababu Rais Thomas Sankara alipenda kushirikiana na mataifa mbalimbali bila kufungamana na upande wowote.Hali iliyopelekea watawala kutoka Ufaransa kukasirika kwani walitaka waendelee kulitawala taifa hilo katika ukoloni mambo Leo kwa kuhakikisha nchi ya Burkinafaso inaendelea kuwa ni soko la bidhaa kutoka Ufaransa na pia bajeti ya matumizi ya Nchi hiyo ikainufaishe nchi ya Ufaransa.Hivyo basi walimtumia rafiki wa Rais Thomas Sankara Bwana Braise Compare kuandaa mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara na hapo ndipo ikawa mwisho wa Rais Thomas Sankara. Tetesi za mauaji dhidi yake Rais Thomas Sankara alizipata, lakini hakuchukua hatua zozote kwani aliamini ubaya usitokee kwake bali utokee kwa wanaompinga.
Tarehe 15/10/1987 Rais Thomas Sankara aliuawa kikatili na kuzikwa usiku huo huo.Na kisha asubuhi yake Bwana Braise Compare rafiki wa karibu wa Rais Thomas Sankara alijitangaza kuwa Rais wa Nchi ya Burkinafaso.Rais Compare alitawala nchi ya Burkinafaso kwa miaka 27 hadi mwaka 2014.
Familia ya Rais Thomas Sankara ilifungua kesi ya mauaji dhidi ya Rais Thomas Sankara ambapo ilipofika mwaka 2022 ilithibitika katika mahakama ya Burkinafaso kuwa Rais Compare na wenzake 14 warishiriki katika mauaji ya Rais Thomas Sankara na Rais Compare alihukumiwa kifungo cha maisha jela.
airdropbulll
May 9, 2025, 8:20
#CHAKUSHANGAZA
Sina shaka kama ni mfuatiliaji wa siasa umeshalisikia jina hili.Thomas sankara alizaliwa tarehe 21/12/1949 huko Yaakov French upper volta (Jina la zamani la Nchi ya Burkinafaso) katika familia ya Bwana Joseph na mama Margaret Sankara ambayo ni familia ya kimisionari.Thomas Sankara alifahamika kwa jina la utani la The African che Guevara kutokana na misimamo yake mikali iliyomfanya akafananishwa na mwanasiasa gwiji kutoka Amerika ya kaskazini Che Guevara.
Kabla ya kuwa Rais wa Nchi ya Burkinafaso Thomas Sankara alihudumu kama waziri Mkuu katika serikali iliyokuwa madarani hadi kufika mwaka 1983 ambapo Thomas Sankara na rafiki yake wa karibu Sana toka wapo jeshini Braise Compare waliongoza mapinduzi ya kiamani kwa kumtoa madarakani Rais aliyekuwepo madarakani kipindi hicho. Rais Thomas Sankara alihudumu madarakani kuanzia mwaka 1983 Hadi mwaka 1987 alipouawa na rafiki yake wa karibu Braise Compare.Mwanamapinduzi na mwanamwema huyu wa Afrika alitawala nchi ya Burkinafaso kwa kipindi cha miaka mitatu na miezi sita.
Katika kipindi chake alipokuwa waziri Mkuu wananchi wa Nchi ya Upper volta jina la zamani la Nchi ya Burkinafaso walikuwa wanavutiwa sana na mtindo wake wa uongozi hali iliyoelekea Rais aliyekuwa madarakani kumuwekea vizuizi Thomas sankara hadi hapo alipofanikiwa kufanya mapinduzi.
MAFANIKIO YAKE KATIKA SERIKALI YA BURKINAFASO
Thomas Sankara ni mmoja wa wanamapinduzi aliyekuwa na maono ya kipekee ya kuivusha nchi ya Burkinafaso kutoka katika mawazo ya utumwa na kuanza kujitegemea kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.Maono yake yalitofautiana na viongozi wengi wa Afrika wa kipindi kile ikiwemo viongozi wenzake katika nchi ya Burkinafaso.
Thomas Sankara mara baada ya kuingia madarakani kama Rais alibadilisha jina la nchi hiyo kutoka kuitwa upper volta la kikoloni na kuiita nchi hiyo jina la Burkinafaso yaani ardhi ya watu wema na wanyoofu.Aidha Thomas Sankara alibadilisha bendera ya nchi hiyo na wimbo wa taifa wa nchi hiyo.
Kwakuwa alidhamiria kuinua uchumi wa Nchi ya Burkinafaso Thomas Sankara alipoingia madarakani alisitisha matumizi makubwa ya serikali kwa vitu visivyo na tija na aliekeza serikali yake itumie gari za kawaida ambazo zitakuwa Hazitumii mafua mengi na gari hizo hazina gharama kubwa.
Rais Thomas Sankara alipoingia madarakani alifanikiwa kuinua kiwango cha ufaulu na uwezo wa kusoma kwa wananchi wa Burkinafaso kutoka asilimia 13 mwaka 1983 hadi asilimia 73 mwaka 1987.
Alianzisha kampeni kabambe ya upandaji wa miti nchi nzima hadi kufikia miti milioni kumi huku akihubiri umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Katika kipindi Cha uongozi wa Rais Thomas Sankara ndipo wanawake wengi zaidi walipata fursa ya kujiunga na jeshi la nchi ya Burkinafaso.
Rais Thomas Sankara alihimiza katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara ambapo hadi kufika mwaka 1987 zaidi ya ekari 3800 zilikuwa zinavunwa mazao ya ngano na mpunga wa kutosha kulisha nchi nzima.
Thomas sankara aliamini kuwa Nchi ya Burkinafaso inaweza kuendelea bila kuchukua mikopo kutoka IMF na world bank ambapo mikopo hiyo mingi ina masharti magumu kwa ustawi wa nchi.
Mwanamapinduzi Thomas sankara hakuweza kuwavumilia wala rushwa waliobainika katika uongozi wake na aliwafukuza mara moja katika serikali.
Rais Thomas Sankara aliamini katika usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume na hivyo katika serikali yake aliyoiunda aliweza kuwapatia nafasi zaidi wanawake sio tu katika wizara inayohusiana na mambo ya wanawake Bali hadi katika wizara nyeti za nchi hiyo tofauto na ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Afrika kwa kipindi hicho.
Rais Thomas Sankara alikuwa muumini mkubwa wa uwazi na demokrasia na mara zote alipenda wananchi wa Nchi ya Burkinafaso watoe maoni yao bila woga wowote tofauti na viongozi wengi wa Afrika wa kipindi kile.